📌Na Mwandishi Wetu,
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari, Jerry William Silaa amewasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi ya siku moja, ambapo amepokelewa rasmi na
mwenyeji wake, Nurdin Babu, Mkuu wa Mkoa huo.
Lengo
kuu la ziara ya Waziri Silaa ni kukagua na kutathmini hali ya upatikanaji wa
huduma za mawasiliano katika Mkoa wa Kilimanjaro, hususan katika eneo la
Mkomazi.
Akizungumza
mara baada ya kuwasili, Silaa amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kila
Mtanzania, popote alipo, anapata huduma bora na ya uhakika ya mawasiliano,
akieleza kuwa mawasiliano ni msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kwa
upande Nurdin Babu, Mkuu wa Mkoa huo amemkaribisha Waziri Silaa kwa niaba ya wananchi wa Kilimanjaro na
kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara hiyo katika kuboresha
miundombinu ya mawasiliano nchini kote.
Katika
ziara hiyo, Waziri Silaa anatarajiwa kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa
wa Kilimanjaro ili kujionea changamoto zilizopo, mafanikio yaliyopatikana,
pamoja na kufanya mazungumzo na wananchi kwa lengo la kupata mrejesho wa moja
kwa moja kuhusu huduma za mawasiliano.
0 Comments