📌BAHATI MSANJILA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amewataka wakandarasi wazawa
kuhakikisha miradi ya miundombinu ya barabara vijijini na mijini inatekelezwa
kwa ubora na ufanisi.
Ameyasema hayo jijini Dodoma, wakati akizindua mafunzo
ya uwezeshaji kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya TARURA kupitia Mfumo wa
Samia Infrastructure Bond.
Mchengerwa amesema kuwa fedha kupitia bond hiyo
zinatosha kutekeleza miradi yote, hivyo hakuna sababu ya miradi kushindwa
kukamilika.
Aidha, amebainisha kuwa Samia Infrastructure Bond ni
suluhisho la changamoto ya mitaji kwa wakandarasi wazawa huku akiitaka TARURA
kuanza kuwalipa wakandarasi 322 waliobaki kuanzia Aprili 11, 2025, baada ya
serikali kuwalipa wakandarasi 457, ili kuwe na usawa na haki kwa wote.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TARURA, Edward Kambona,
amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na CRDB na wakandarasi wazawa
kukamilisha miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
0 Comments