📌BAHATI MSANJILA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza kuwa
kupitia Bunge Marathon 2025, Bunge linatarajia kukusanya Sh bilioni 3 kwa ajili
ya ujenzi wa shule ya wavulana ya Bunge itakayojengwa Kikombo, Dodoma.
Akizungumza kwenye uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma, Majaliwa amesema shule hiyo itakuwa ya kisasa yenye miundombinu yote
kama madarasa, mabweni, maabara, nyumba za walimu na viwanja vya michezo.
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema hii ni
marathon pekee inayojumuisha Wabunge wote wa majimbo 264, na inalenga kuleta
mabadiliko ya kweli kwenye elimu ya mtoto wa kiume.
Dkt. Tulia Ackson amewashukuru wadau mbalimbali
kwa mchango wao katika kufanikisha mpango wa ujenzi wa shule ya wavulana ya
Bunge kwa ngazi ya kidato cha tano na sita.
Mwenyekiti wa Bunge Marathon 2025, Festo Sanga
ambaye pia ni Mbunge wa Makete, Sanga ameeleza kuwa mbio hizo za hisani ni zao
la maono ya Spika Tulia Ackson, zikiwa na lengo la kuendeleza jitihada za
maendeleo ya elimu kwa watoto wa kiume baada ya kukamilisha shule ya wasichana.
Zaidi ya wakimbiaji 5,000 wamejitokeza kushiriki
mbio hizo za hisani, zikiwa ni mwendelezo baada ya ujenzi wa shule ya wasichana
ya Bunge.
0 Comments