BUNGE HALIJAPITISHA SHERIA YA KUWA WAKULIMA WAMILIKI WA MASHINE ZA EFD” — WAZIRI BASHE

 




Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema kuwa hakuna sheria iliyopitishwa na Bunge inayowataka wakulima, hususan wa vijijini, kumiliki mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD) bali ni kwa wafanyabiashara waliotakiwa kuwa na leseni za biashara na TIN namba

Akijibu Hoja zilizoibuliwa na Wabunge mbalimbali kwa bajeti iliyosomwa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kwa wizara hiyo na taasisi zilizo chini yake Waziri Bashe amesema kumekuwa na kilio kutoka kwa wakulima waliolalamikia kushinikizwa kuwa na mashine hizo.

kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema baadhi ya miradi ya maji haikukamilika awali kutokana na ufinyu wa bajeti lakini chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, jumla ya miradi 177 imekamilika na sasa inatoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imekamilisha tathmini ya athari zitakazojitokeza kufuatia kusitishwa kwa baadhi ya ufadhili kutoka Serikali ya Marekani huku akieleza kuwa tayari Serikali imechukua hatua za kufidia fedha hizo ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi haukwami.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga, akijibu hoja kuhusu malengo ya kimataifa ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030, amesema hakuna jambo litakaloshindikana kwa sababu Serikali imejipanga kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments