📌Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry William Silaa , ameshiriki zoezi la
kupandisha vifaa vya ujenzi wa Mnara wa Mawasiliano katika kijiji cha Idete,
Kata ya Chanzuru, Kilosa, Mkoani Morogoro.
Mnara huu ni miongoni mwa minara 758 ya
Mawasiliano inayojengwa na Serikali kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali,
kwa lengo la kuboresha huduma za mawasiliano katika vijiji vya mbali na maeneo
yenye changamoto za miundombinu.
Kati ya minara 758 inayojengwa katika maeneo
mbalimbali nchini, minara 69 inajengwa katika Mkoa wa Morogoro, ambapo minara
26 ipo katika hifadhi mbalimbali na mbuga za wanyama.
Kwa upande wa Wilaya ya
Kilosa pekee imenufaika kwa kupata minara 17.
Aidha, kuwepo kwa mnara wa simu katika Kijiji
cha Idete unaojengwa na Kampuni ya Simu ya Airtel kutasaidia kupunguza
changamoto za huduma za mawasiliano katika kijiji hicho na kunufaisha wananchi
zaidi ya 7,000, hivyo kuboresha shughuli za kijamii na kiuchumi.
Akitoa taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda amesema kuwa mnara
huo unatarajiwa kukamilika na kuwashwa tarehe 1 Aprili, 2025 na kukabidhiwa
rasmi tarehe 15 Aprili, 2025.
Ameongeza kuwa, hadi sasa, jumla ya minara 420
kati ya 758 imekamilika na inatoa huduma. Hii ni sawa na asilimia 55 ya
utekelezaji wa mradi huo.
0 Comments