📌Na MWandishi wetu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewasilisha tamko la Tanzania kuhusu
maendeleo ya nchi katika kufikia usawa wa kijinsia kwa kurejea Maazimio ya
Beijing.
Waziri Dkt. Gwajima amewasilisha tamko hilo akiwa
ni miongoni mwa Mawaziri wa nchi mbalimbali duniani waliowasilisha matamko
rasmi ya nchi zao kwenye kipindi cha ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Hali
ya Wanawake Duniani (CSW69), tarehe 13 Machi, 2025, Jijini New York Marekani.
Katika tamko hilo Waziri Dkt. Gwajima amesema
katika utekelezaji wa maazimo ya Mkutano wa Beijing Tanzania imeongeza
kwa idadi ya Viongozi Wanawake akimtaja Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kama mfano dhahiri katika hilo.
Amewataja Viongozi wengine wanawake kuwa ni pamoja
na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Naibu Spika wa Bunge la
Wawakilishi Zanzibar na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzbar.
Aidha, pia alisema, kuna ongezeko la Wanawake Mawaziri, Wabunge,
Makamisha, Majaji, Mabalozi na Madiwani.
Dkt Gwajima ameeleza kwamba Sera ya elimu na
mafunzo toleo la mwaka 2023 na mikakati yake imewezesha uwiano wa kuandikisha
watoto shule za msingi kufikia 1:1 kati ya wasichana na wavulana, pamoja na
Utekelezaji wa mikakati ya msingi na kina kwenye eneo la Wanawake na Afya
ambapo vifo vitokanavyo na sababu za uzazi kwa wanawake vimepungua kutoka vifo
556 hadi 104 kwa vizazi hai 100,000.
Ameongeza kwamba Programu ya Afrika ya
Wanawake na Nishati Safi ya Kupikia iliyozinduliwa kwenye Mkutano wa COP 28
chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kama kinara, na
utekelezaji wa Mkakati kuhusu Nishati Safi ya Kupikia wa Mwaka 2023 -2033
unalenga asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia
ifikapo mwaka 2034.
Dkt. Gwajima amesisizitiza kwamba Tanzania
imeboresha Sheria mbalimbali zikiwemo Sheria ya Msaada wa Kisheria, Sheria ya
Makosa ya Mtandao na Sheria ya Mtoto ili kuwalinda Wanawake, Wasichana na
Watoto. Pamoja na kuwa na sheria ya uchaguzi ili kupambana na ukatili dhidi ya
Wanawake wakati wa uchaguzi na Vyama vyote vya Siasa.
Aidha, amesema tangu mwaka 2023 Tanzania
inatekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ambayo, imeshafikia
watu milioni 1.3 huku nusu wakiwa ni Wanawake.
0 Comments