📌BAHATI MSANJILA
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeahidi
kuhakikisha jumuiya hiyo inachochea ushindi wa kishindo kwa CCM kuelekea
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa kuandaa midahalo mbalimbali ili kueleza
mafanikio yaliyopatikana chini ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Ili kufanikisha
hilo, UVCCM imewataka vijana kushiriki kikamilifu na kuhamasisha wenzao
kushiriki maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili wapate haki ya
kupiga kura kwenye uchaguzi ujao.
Katibu wa Idara ya
Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifa, Jessica Mshama, ametoa ahadi hiyo
jijini Dodoma baada ya kupokelewa rasmi katika Makao Makuu ya jumuiya hiyo.
Amesema vijana wanapaswa kuwa mabalozi wa Taifa kwa kuchagua viongozi wenye utu
badala ya wale wenye uchu wa madaraka.
Akizungumza katika
hafla hiyo, Mkuu wa Utawala na Uendeshaji wa UVCCM Makao Makuu, Amina Kaumo, na
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Abdulhabib Mwanyemba, wameahidi
kushirikiana kikamilifu kuhakikisha kura za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
zinapatikana kwa wingi.
Katibu huyo
aliteuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kushika nafasi hiyo
Februari 21 mwaka huu, na sasa anajipanga kuimarisha uhamasishaji wa vijana
kuelekea uchaguzi.
0 Comments