📌BAHATI MSANJILA
Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote (UCSAF) umeendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini kwa kusimika
jumla ya minara 148 katika Kanda ya Kati, ambapo 78 kati
yake tayari imewashwa na inafanya kazi.
Kwa mujibu wa
taarifa kutoka UCSAF, mikoa iliyofaidika na mpango huu ni Dodoma
Minara 36 na 25 imewashwa, Singida 32 minara, 14 imewashwa, Iringa 22 minara,
10 imewashwa, Tabora 50 minara, 23 imewashwa, na Kigoma 8 minara, 6 imewashwa.
Mpango huu ni sehemu
ya jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wote, hususan walioko vijijini,
wanapata huduma bora za mawasiliano, hivyo kuwezesha maendeleo ya kijamii na
kiuchumi kupitia teknolojia ya mawasiliano.
0 Comments