📌Na Mwandishi wetu
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema treni ya mwendo kasi ya mizigo itaanza kazi mwishoni mwa Mei 2025, ikihudumu kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Mateshi Tito,
amesema tayari mabehewa 264 ya mizigo yamewasili nchini na kufanyiwa
majaribio.
Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa 39 wa
Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT), ambapo wajumbe walishiriki katika ziara ya
NMB ALAT SGR Royal Tour kati ya Dodoma na Dar es Salaam, chini ya udhamini wa
Benki ya NMB.
Mhandisi Tito pia ameeleza kuwa tangu treni ya
mwendo kasi ya SGR ianze safari zake Julai 2024, hadi Machi 2025, tayari
imesafirisha abiria milioni mbili.
Afisa mkuu wa wateja
wakubwa na serikali Benki ya NMB Alfred Shayo amesisitiza umuhimu wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa katika kukuza uchumi wa nchi na wananchi mmoja mmoja.
Kutokana na hilo, wameamua
kuwa wadhamini wakuu wa mkutano huo na kutumia Royal Tour hiyo kutoa elimu ya
fedha kwa wajumbe wa ALAT, ili nao wawafundishe wananchi wanaowaongoza.
0 Comments