TARURA YAFUNGUA BARABARA MPYA KM. 8.24 WILAYANI MOMBA

 





Na Mwandisi Wetu

Kwa mara ya kwanza wananchi wa Kata ya Mpemba na Mpande wananufaika na kufurahia matunda ya ujenzi wa barabara itakayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi na Maisha yao kwa ujumla.

Mhandisi Yusuph Shabani Meneja TARURA Wilaya ya Momba ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma amesema wamejenga barabara ya Mpande - Katenjele inayounganisha Kata hizo.

Amesema barabara hiyo ina urefu wa Km. 8.24 na tayari imekamilika na imejengwa na Mkandarasi HSS ENGINEERING kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.

Mhandisi Yusuph amebainisha wana jumla ya Halmashauri mbili wanazozihudumia ambazo ni Halmashauri ya Mji Tunduma na Halmashauri ya Wilaya Momba .

Amesema eneo hilo la ukanda wa chini ndio eneo lenye changamoto kubwa kutokana na jiografia yake kuwa na mito mingi na mikubwa inayopeleke maji katika Ziwa Rukwa,"na barabara zipo katika hali ambayo tumeendelea kupambana nazo kuhakikisha zinapitika katika kipindi chote cha mwaka.

Ameongeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba wamekuwa na miradi mikubwa miwili ya kimkakati, mradi wa kupunguza mlima mkali barabara ya Ikana –Makamba, ili kuhakikisha tunafungua mawasiliano kati ya eneo la Ukanda wa juu na chini


Kwa upande wa Mji wa Tunduma mjini wameweza kupambana kwa fedha za mafuta, Jimbo na maendeleo ambapo wameweza kujenga barabara za lami yenye jumla ya urefu wa Km. 10.27.






Post a Comment

0 Comments