TANESCO KUANZISHA MKOA MAALUM WA SGR ILI KUBORESHA HUDUMA YA UMEME

 


        

📌BAHATI MSANJILA


MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amesema Shirika hilo lipo mbioni kuanzisha mkoa wa kitanesco wa njia ya treni ya umeme (SGR) ambao utakuwa na kazi moja tu ya kushughulikia njia ya treni hiyo ili kuondoa changamoto za kuzimikazimika njiani.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Gissima Nyamo -Hanga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya shirika hilo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita. 

Amesema hatua hiyo ni kufuatia changamoto zilizojitokeza awali za kukatika kwa umeme katika treni hiyo kipindi Cha awali treni hiyo ilipoanza safari zake.

Akielezea mafanikio ya Shirika hilo ndani ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita Mhandisi Nyamo hanga amesema ni kuongezeka kwa hali ya uzalishaji umeme.

Aidha amesema,Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya kuimarisha grid ya Taifa (Grid imara ) kwa lengo la kuimarisha
miundombinu ya njia za kusafirisha umeme na kusambaza umeme, kupanua vituo vya kupoza umeme, kujenga njia mpya za kusafirisha umeme.

Pia lengo la mradi huo ni kufanya Ujenzi wa vituo vya kupoza umeme, ubadilishaji wa nguzo za miti kusimika za zege na ufungaji wa transfoma ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mfumo wa Gridi ya Taifa .

Amesema, utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 40 ambapo miradi sita kati ya 27 imekamilika na unategemewa kukamilika mwaka wa fedha 2026/2027.







 

Post a Comment

0 Comments