Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwakushirikiana na Benki ya NMB imeboresha mfumo
wa uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha katika vituo vya huduma ili
kuhakikisha usalama wa fedha na kuharakisha utoaji wa huduma kwa jamii.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Adolf
Ndunguru, amesema hayo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya matumizi
ya Bank Mtandao kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Serikali za
Mitaa, Angelista Kihoga, ameeleza kuwa mfumo huo utasaidia kupunguza muda na
gharama sambamba nakusaidia ufutaliaji wa mapato.
Naye, Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali
kutoka NMB, Bi. Vicky Bishubo, amesema mfumo huo utarahisisha ukaguzi na uwazi
wa fedha, akibainisha kuwa benki hiyo ilifanya majaribio kwenye halmashauri 10
na kufikia Desemba 2024, shule na vituo vya afya zaidi ya 1,000 vilikuwa
vimeunganishwa na huduma ya Internet Banking.
0 Comments