📌BAHATI MSANJILA
Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, ameagiza kukamilika kwa
ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini ifikapo Mei 12, 2025, na
kuhakikisha yote imewashwa ili wananchi waanze kunufaika na huduma za
mawasiliano.
Akizungumza
katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo katika Kijiji cha Kidete, Wilaya ya
Kilosa, Morogoro, Waziri Silaa amesema kuwa Serikali imetenga Shilingi bilioni
126 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, ambao utapunguza changamoto ya
mawasiliano nchini.
Amesisitiza
kuwa mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa
Kidijitali (2024-2034) uliozinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ukiwa na
lengo la kuboresha miundombinu ya mawasiliano.
Hadi
sasa, minara 420 kati ya 758 imekamilika, ikiwa ni zaidi ya asilimia 55 ya
utekelezaji wa mradi huo, ambao unatarajiwa kunufaisha wananchi milioni 8.5
waishio vijijini.
0 Comments