📌BAHATI MSANJILA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa amefurahishwa na mwitikio wa taasisi za Serikali kwa kutenga na kutoa asilimia 30 ya bajeti za ununuzi kwa ajili ya makundi maalum katika jamii.
Rais Samia ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika kitaifa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, 8 Machi 2025, jijini Arusha.
Alisema jambo hilo limewezekana kupitia sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 iliyoweka sharti kwa taasisi nunuzi kutenga asilimia 30 ya zabuni zote kwa ajili ya makundi maalum ikiwa ni pamoja na wanawake.
Nimefurahishwa sana juzi nikiwa napokea taarifa ya Sekta ya Ujenzi na Miundombinu wakaniambia kwamba kuna kazi kadhaa za barabara zimetolewa, na asilimia 30 ya kazi hizo wamepewa wakandarasi wanawake,a
Pia, alieleza kuwa makundi 66 ya wanawake yalipata zabuni 146 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 5.6, na kwamba kiasi kilichobaki kimeenda kwa makundi mengine.
0 Comments