📌BAHATI MSANJILA
Wananchi wa kata ya Rorya wilaya ya Tarime mkoani Mara wameishukuru benki ya NMB kwa kuwaletea elimu ya fedha hadi kwenye vijiji vyao na kuwaakikishia kila kijiji nchi nzima kutakuwa na mawakala wa benki hiyo wasiopungua wawili.
Wananchi hao wa kata ya Rorya wametoa shukrani
hizo kwa benki ya NMB wakati wa bonanza la NMB KIJIJI DAY, lililofanyika katika
kijiji cha Minigo kata ya Rorya wilayani Tarime, bonanza ambalo linahusisha
utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi wa maeneo husika pamoja na vikundi
mbalimbali vya wajasiriamali vilivyopo ndani ya kata hiyo.
Kwa upande wao benki ya NMB Kupitia meneja wa kanda ya ziwa Faraja Ng’ingo wanasema lengo la NMB kijiji day ni kuhakikisha kila kijiji nchi nzima wanawafikia kwa kuwapa elimu ya fedha pamoja na kuwawezesha kupata mawakala wa NMB wasiopungua wawili, na katika kuhakikisha wanafanikisha hilo kila mwezi wanavifikia vijiji 250 kwa kuwapa elimu ya fedha kupitia mtu mmoja mmoja na vikundi vya wajasiriamali ndani ya kijiji husika.
Aidha katika kampeni hiyo ya NMB KIJIJI DAY,
benki ya NMB wanaambatana na kampuni ya nishati safi ya kupikia ya Taifa gas
ambayo kupitia mkusanyiko huo wamekuwa wakitoa elimu ya matumizi ya nishati
safi ya kupikia, ikiwa ni kuunga mkono jitihada ya serikali ya kuhakikisha
ifikapo 2030 watanzania zaidi ya asilimia 80 wawe wanatumia nishati safi.
Lengo la benki ya NMB kuanzisha kampeni ya NMB
KIJIJI DAY ni kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha kila mtanzania
popote pale alipo anafikiwa na huduma za kifeda (financial inclusion), na hivyo
kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja.
0 Comments