NGORONGORO YAVUTIA WATALII MILIONI 2.9, MAPATO YAONGEZEKA

 


📌BAHATI MSANJILA

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeripoti ongezeko kubwa la watalii, ambapo kati ya Julai 2021 na Februari 2025, idadi ya wageni waliotembelea hifadhi hiyo imefikia milioni 2.9  huku mapato yakivuka shilingi bilioni 693.

 

Taarifa hiyo imetolewa na kamishina wa uhifadhi wa Ngorongoro Dkt. Elirehema Doriye ambaye amesema fedha hizo zimeingizwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya utalii na uhifadhi nchini.

 

Kwa mujibu wa Dkt. Doriye, mwaka wa fedha 2024\2025 unaashiria ongezeko zaidi la watalii, ambapo Mamlaka ilikadiria kukusanya shilingi bilioni 230, lakini tayari asilimia 92 ya lengo hilo imeshafikiwa.

 

Dkt. Doriye ameeleza kuwa, mbali na juhudi za matangazo ya utalii, ushirikiano kati ya sekta binafsi na mamlaka za utalii umechangia ongezeko la wageni. Ili kuboresha huduma, Mamlaka ya Ngorongoro inaendelea kufanya maboresho yafuatayo:

 

Aidha, kati ya Januari 2021 na Februari 2025, Serikali imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya barabara na maji ili kuboresha mazingira ya uhifadhi ndani ya hifadhi na maeneo yanayoizunguka.

 

Kuhusu mpango wa kuhamisha watu kwa hiari kutoka Ngorongoro, Dkt. Doriye amesema kuwa ongezeko la idadi ya watu na mifugo limeleta changamoto kubwa katika uhifadhi.

 

Kutokana na ongezeko hilo, kulikuwa na changamoto za uhifadhi na ustawi wa wakazi. Ili kulinda maisha yao na kuwaondoa katika hatari ya kuishi na wanyamapori, Serikali ilianzisha mpango wa uhamaji wa hiari kwenda Msomera, Handeni, Tanga.

 

Serikali pia imejenga nyumba 3,003 kwa ajili ya wahamaji, ambapo nyumba 1,495 zimekwishakaliwa na 1,508 ziko tayari, zikisubiri kukamilika kwa miundombinu ya kijamii.






Post a Comment

0 Comments