📌Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi amepongeza uwepo kwa huduma bora za mawasiliano ya simu na intaneti katika eneo la forodha lililopo katika mpaka wa Tunduma.
Naibu Waziri Mahundi ametoa pongezi hizo wakati wa
ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano maeneo ya mipakani
leo, Machi 21, 2025, katika mpaka wa Tunduma mkoani Songwe.
Mhe. Mahundi ametumia fursa hiyo kuisisitiza
kampuni ya Airtel Tanzania kukamilisha ujenzi wa mnara wa mawasiliano ya simu
kupitia Mradi wa Tanzania Kidijitali katika Wilaya ya Momba, hasa katika Kata
ya Nzoka, Kijiji cha Namtambala, ili kuboresha huduma za Mawasiliano katika
eneo husika.
Akitoa salamu, Mkuu wa Wilaya ya Momba, Elias
Mwandobo, ameipongeza wizara kwa juhudi zake katika kuboresha huduma za
mawasiliano, pamoja na kutoa rai kwa wananchi kutumia huduma hizi ili kujipatia
maendeleo, ikiwemo sekta ya kilimo.
Naye, Bw. Nsajigwa Mwambegele, Meneja Msaidizi wa
Idara ya Forodha Mkoa wa Songwe, ameishukuru serikali kupitia Wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuwezesha huduma bora katika eneo hilo.
0 Comments