Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mohammed
Mchengerwa amempa mkandarasi anayejenga jengo la TAMISEMI katika Mji wa
Serikali Mtumba, Dodoma miezi miwili kuhakikisha anakamilisha ujenzi, ili
ifikapo Juni Mosi mwaka huu jengo hilo lianze kutumika rasmi.
Waziri Mchengerwa ametoa agizo hilo jijini Dodoma
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Mchengerwa amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha
kazi inafanyika kwa ufanisi usiku na mchana bila visingizio vyovyote.
Kwa upande wake, Mkandarasi anayetekeleza mradi
huo kutoka Vikosi vya Ujenzi, Mhandisi Deogratius Japhet, ameahidi kutekeleza
agizo hilo na kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.
0 Comments