📌Na Mwandishi Wetu,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa,
amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa
Pwani, Mhandisi Leopold Runji, kuhakikisha wakandarasi wanakamilisha ujenzi wa
barabara za lami Ikwiriri ndani ya miezi miwili ili wananchi wanufaike na
maboresho ya miundombinu hiyo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya
kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo wilayani Rufiji.
Ameagiza Meneja wa TARURA kuwasimamia wakandarasi wafanye
kazi usiku na mchana, akibainisha kuwa barabara hizo zilipaswa kukamilika
Desemba 2024 na iwapo hazitakamilika kwa muda uliopangwa, atamuwajibisha meneja
huyo.
Nao, Baadhi ya wananchi, akiwamo Dereva wa bodaboda Ramadhan
Mwipi na Mama Lishe Mariam Hamza, wamemshukuru Waziri Mchengerwa na Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha barabara hiyo, wakieleza kuwa imeleta ahueni
kubwa kwa usafiri na biashara zao.
0 Comments