Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali
za Mitaa (LAAC), imeielekeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mlimba kuhakikisha inazingatia miongozo na kanuni katika utekelezaji wa miradi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Halima Mdee ametoa
maelekezo hayo baada ya ukaguzi wa miradi miwili ambayo ni nyumba ya Mkurugenzi
wa Halmashauri na kukagua mradi wa wodi tatu (wanaume, wanawake, na watoto)
katika hospitali ya Halmashauri.
Amesema kamati imeongeza kuwa matumizi sahihi ya
miongozo, sheria, na kanuni ni muhimu katika kuhakikisha miradi inatekelezwa
kwa kuzingatia thamani ya fedha na kuepusha matumizi mabaya ya rasilimali.
Naye, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI,
Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa ofisi yake imepokea maelekezo hayo na
tayari imeanza kuyafanyia kazi kwa utekelezaji.
0 Comments