KASI YA UJENZI WA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU ARUSHA YAIVUTIA KAMATI YA BUNGE

 


 


📌Na mwandishi wetu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imevutiwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa Miguu Arusha ambao ujenzi huo upo mbele ya muda kwa kufikia asilimia 33 badala ya asilimia 31 iliyotarajiwa hadi sasa. 

Kauli hiyo imetolewa  jijini Arusha na Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Husna Sekiboko wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Arusha ambao unatarajiwa kutumika katika michuano ya AFCON 2027. 

Aidha, Kamati hiyo imeitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea na kasi hiyo ya utekelezaji wa mradi huo ili uwanja ukamilike kwa wakati na tija iliyokusudiwa. 

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema ujenzi wa uwanja huo umefikia asilimia 33 na utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 32,000 utakapokamilika June 2026, huku akieleza kuwa uwanja huo utakuwa uwezo wa kudumu miaka 130 ukiambatana na marekebisho ya kila baada ya miaka 10.







Post a Comment

0 Comments