HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YAWEKA REKODI KATIKA MATIBABU YA NGUVU ZA KIUME

 



📌BAHATI MSANJILA


Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imefanikiwa kuweka vipandikizi maalum kwenye uume kwa wanaume watano waliokuwa na changamoto za upungufu wa nguvu za kiume, ikiwa ni hospitali ya kwanza kutoa huduma hiyo hapa nchini.

 

Amesema hayo jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio na mwelekeo wa hospitali hiyo kuelekea miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Abel Makubi, kati ya asilimia 40 hadi 50 ya wanaume wanakabiliwa na tatizo la nguvu za kiume.

 

Profesa Makubi amesema kuwa ndani ya miaka mitatu ijayo, hospitali hiyo inatarajia kuanza kutumia roboti ili kuongeza usahihi wa matibabu, hatua inayolenga kuboresha zaidi huduma za kibingwa.

 

Hospitali ya Benjamin Mkapa, iliyozinduliwa rasmi Oktoba 2015, imehudumia jumla ya wagonjwa 972,740 katika kipindi cha miaka minne, huku kiasi cha Shilingi bilioni 36.95 kikiwa kimewekezwa ili kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.

 

Aidha, kupitia mkakati wa 4R wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, huduma za kibingwa hospitalini hapo zimeongezeka kutoka 14 hadi 20, huku huduma za ubingwa wa juu zikiongezeka kutoka 7 hadi 16.






Post a Comment

0 Comments