📌Na Mwandishi Wetu,
Katibu Mkuu wa Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amepokea ugeni kutoka
Shirika la Watoto la SOS Children's Village ambapo ugeni huo ukiongozwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Aisha Salim Ali katika Ofisi za Wizara
jijini Dodoma.
Dkt Jingu amelipongeza Shirika hilo kwa jitihada
zake za kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanadhibiti changamoto ya
watoto kuishi na kufanya kazi mitaani baada ya Shirika hilo kukabidhi Mwongozo
wa Taifa wa Uanzishaji, Uendeshaji na Usimamizi wa makao ya watoto nchini.
Aidha Dkt. Jingu ametoa wito kwa jamii
kuimarisha taasisi ya familia na kuepuka migogoro kwani tafiti zinaonesha hivi
karibuni kumekua na kuvunjika kwa ndoa nyingi na kupelekea kupatikana kwa wimbi
la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SOS
Children's Village Aisha Salim Ali ameahidi ushirikiano kati ya Shirika lake na
Wizara katika kuhudumia Watoto katika Makao ya Watoto kwa kuweka namna nzuri ya
Utoaji wa huduma na Malezi katika Makao hayo.
0 Comments