📌BAHATI MSANJILA
Washindi sita wa draw kubwa na ya mwisho ya kampeni ya MASTABATA msimu
wa sita wamekabidhiwa tiketi zao za kwenda na kurudi nchini Dubai kwa siku
tano, huku gharama zote za safari hiyo zikilipiwa na benki ya NMB kwa
kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya kadi za malipo ya MASTER CARD.
Aidha washindi hao sita, na wenza wao au mtu anaemchagua kuambatana nae kwenye
safari hiyo, jumla yao kumi na wawili, wamepata tiketi hizo baada ya kushinda
kwenye draw ya mwisho ya kampeni ya MASTABATA LA KIBABE ambayo inaendeshwa na
benki ya NMB kila mwaka.
Akiongea muda mfupi kabla ya kukabidhi tiketi hizo kwa washindi hao sita wa
MASTABATA Msimu wa sita, Afisa mkuu wa biashara na wateja binafsi wa benki ya
NMB Filbert Mponzi amesema katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda miezi mitatu
na ambayo ilitengewa jumla ya sh million mia tatu.
Amesema jumla ya washindi 1256
walijinyakulia zawadi mbalimbali, ikiwamo washindi kumi waliolipiwa ada za
shule ambapo kila mmoja alipata million nne, washindi 30 kila mmoja
alijinyakulia sh laki tano, na washindi kumi ambao walifanya utalii wa ndani
kwa kwenda mbuga ya wanayama ya mikumi na Ngorongoro.
Mponzi amesema katika kipindi cha kampeni ya MASTABATA LA KIBABE iliyodumu kwa miezi mitatu pamoja na mafanikio mengine yaliyopatikana, wateja wanatumia njia za kidigitali katika kufanya manunuzi waliongezeka kwa asilimia 27.
Kampeni ya MASTABATA LA KIBABE lengo lake ni kuendelea kujenga utamaduni kwa watanzania wa kupenda kutumia njia za kidigitali katika kufanya manunuzi ikiwamo NMB MASTERCARD, QR CODE, NMB Mkononi pamoja na Biashara za mtandaoni.
0 Comments