📌BAHATI MSANJILA
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bara Steven Wasira, amewataka wanawake nchini kuhakikisha wanazingatia maadili bora na malezi mema kwa watoto wao, huku akisisitiza kuepuka maadili mabovu, ikiwa ni pamoja na kuhusisha mapenzi ya jinsia moja.
Wasira ameyasema hayo jijini dodoma wakati
akizungumza kwenye kongamano kuelekea maadhimisho ya miaka 48 ya Chama cha
Mapinduzi CCM lililoandaliwa na Umoja wa wanawake Tanzania (UWT).
Wasira amekumbusha maneno ya Rais Yoweri Kaguta
Museveni wa Uganda aliyosema kuhusu mapenzi ya jinsia moja, akisema kuwa iwapo
atakutana na wanaume wanaoshirikiana kimapenzi, atawafunga jela na kuwaondoa
kama wanaume, akielezea kuwa hali hiyo ni kinyume na maumbile na haiwezi
kukubalika.
Katika hotuba yake, Wasira amewataka wanawake kuwa
macho na kuhakikisha wanalea watoto kwa misingi bora ili kuwaepusha na
ushawishi wa maadili mabaya.
Akiendelea,amesisitiza kuwa, “Wamejaribu
kutuharibu, lakini hatukubaliani nao Mke na mke wakioana hawawezi kuzaa, na
mume na mme wakioana hawawezi kuzaa.
Wasira amekumbusha kuwa CCM itaendelea kuongoza
kwa imani ya Watanzania na kwamba wataendelea kutunza amani na kuimarisha
maendeleo ya nchi. Alisema, “Msiwache watoto wetu wakaharibike, mzingatie
malezi na mhakikishe nchi yetu inaendelea kuwa nchi bora.”
Akizungumzia mchango wa Rais Samia Suluhu Hassan
katika maendeleo ya Tanzania, Wasira amesema Rais Samia amefanya kazi nzuri
katika kipindi cha uongozi wake, na amevunja rekodi katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa utekelezaji mzuri wa
Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2024.
Kwaupande wake makamu mwenyekiti UWT Zainab
Shomari amesema kuwa UWT ni jeshi kubwa la kweli, likiwa na idadi kubwa ya
wanawake kutoka sehemu
mbalimbali nchini.
0 Comments