📌BAHATI MSANJILA
Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Imesema katika kuadhimisha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita imejipanga kutekeleza miradi 113 yenye thamani ya Sh.bilioni 11.3 kwa mwaka wa Fedha 2024/25.
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Erasmus Kipesha ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo 113 wanafunzi 19,482 na walimu 12 watanufaika na miradi hiyo.
Pia amefafanua kuwa TEA inasimamia
mifuko miwili ambao ni mfuko wa kuendeleza ujuzi na mfuko wa elimu ambapo
katika kipindi cha miaka minne ya Awamu ya Sita, imepokea kiasi cha Sh.bilioni
49.05 kwa ajili ya mfuko wa elimu.
Amesema kiasi cha Sh. bili 2.8 zilipelekwa kwenye mfuko wa kuendeleza ujuzi na kiasi Cha shilingi bilioni 4.11 zilitoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Elimu katika Mamlaka hiyo.
Pia eneo lingingine la kipaumbele ni katika vifaa vya kufundishia na kujifunzia ikiwemo vitabu vya kiada na zana nyingine za kufundishia ,upatikanaji wa vifaa vya TEHAMA na kufunga mitandao ,vifaa saidizi kwa wenye mahitaji Maalum ,programu Maalum kuwezesha wanafunzi wa kike na mikopo kwa ajili ya ujenzi ,upanuzi na ukarabati wa majengo vyuo vikuu vya Elimu ya juu.
Akizungumzia idadi ya watu walionufaika na mfuko wa kuendeleza ujuzi Kaimu Mkurugenzi Utafutaji na Usimamizi wa Miradi ya Elimu TEA Masozi Nyirenda amesema, takribani watanzania 49,000 wamenufaika huku wanawake wakiwa ni zaidi ya 2,000, Makundi maalum 474, kaya maskini 4,000 na 600 kutoka Zanzibar.
0 Comments