📌BAHATI MSANJILA
Serikali wilaya ya
Kilosa imesema benki ya NMB imekuwa ikifanya vizuri na ni taasisi ya kuigwa
katika kujenga mahusiano yake na jamii zinazowazunguka na serikali kwa
ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka
amebainisha hayo Kijiji cha Msowero wilayani Kilosa wakati anafungua NMB Kijiji
Day, ambapo katika siku hiyo benki ya NMB inafanya michezo mbalimbali na
wanakijiji husika, kutoa elimu ya fedha kwa wananchi na vikundi vya
wajasiriamali katika eneo hilo lengo la Kijiji day likiwa kila mtanzania popote
pale alipo awe na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya fedha na kunufaika na
fursa zinazotolewa na taasisi za kifedha hapa nchini
Mkuu wa Wilaya Shaka amesema ni ukweli
usiopingika kuwa benki ya NMB imekuwa ikigusa Maisha ya watanzania hadi yule wa
chini kabisa kutokana na mifumo yake ya urejeshaji kwa jamii ilivyojiwekea,
ambapo katika NMB Kijiji Day kijijini MSOWERO licha ya kutoa elimu ya fedha na kufungulia
wananchi akaunti, pia waliambatana na kampuni za zana za kilimo na nishati safi
ya kupikia ambao nao pia walitoa elimu kwa wanavijiji hao.
Kwa upande wao benki ya NMB kupitia meneje wa
NMB kanda ya Kati Janeth Shango Amesema NMB Kijiji Day ambayo lengo lake kuu ni
kuhakikisha kila mtanzania popote pale alipo anapata elimu ya fedha, wamekuwa
wakitumia siku hiyo pia kutoa elimu ya masuala ya utawala bora, bima , kilimo
biashara pamoja na mikopo kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali vilivyopo vijijini.
Benki ya NMB imeanzisha kampeni maalumu
inayoitwa NMB KIJIJI DAY lengo likiwa kuhakikisha hakuna mtanzania anaeachwa
nyumba katika kupata elimu ya fedha, na katika kampeni hiyo pia benki ya NMB
inahakikisha kila Kijiji hapa nchini kinakuwa na MAWAKALA WA BENKI YAKE
wasiopungua wawili ili dhana nzima ya huduma za kifedha jumuishi liweze
kufanikiwa kwa vitendo.
0 Comments