MAELFU YA VIJANA WAJITOKEZA KUSHIRIKI CCM @48 MARATHON KUDUMISHA MAADHIMISHO YA MIAKA 48 YA CCM

 


📌BAHATI MSANJILA

Maelfu ya vijana wamejitokeza jijini Dodoma kushiriki CCM @48 Marathon, ikiwa ni sehemu muhimu ya maadhimisho ya miaka 48 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mbio hizi zinahitimishwa katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, huku Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella, akiongoza shughuli za CCM Marathon, ikiwa ni muendelezo wa maandalizi kuelekea maadhimisho ya miaka 48 ya chama hicho.

Viongozi wengine walioshiriki mbio hizo ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Kawaida, Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo, na Katibu wa NEC Organization, Issa Gavu.

Mwenyekiti wa Chama Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutimiza miaka 48 ya CCM, itakayofanyika tarehe 5 Februari 2025.







Post a Comment

0 Comments