📌BAHATI MSANJILA
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Kawaida,
amekagua maandalizi ya CCM @48 Marathon yanayofanyika Dodoma, ikiwa ni sehemu
ya Maadhimisho ya Miaka 48 ya CCM. Kawaida amewataka vijana kujitokeza kwa
wingi kushiriki mbio hizo, akisisitiza kuwa maandalizi yamekamilika na wataweza
kupokea zaidi ya vijana 15,000 watakaoshiriki.
Amesema kuwa mbali na mbio, kutakuwa na shughuli
mbalimbali za burudani, ikiwa ni pamoja na furaha, michezo, na nyimbo, zote
zikienda sambamba na maandalizi kuelekea tarehe 5 Februari 2025, ambapo CCM
itaadhimisha miaka 48 tangu kuanzishwa kwake.
Mgeni rasmi katika mbio hizo anatarajiwa kuwa Katibu
Mkuu wa CCM, na mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Emmanuel Nchimbi.
Mwenyekiti wa Chama Taifa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
hafla ya kutimiza miaka 48 ya CCM, itakayofanyika tarehe 5 Februari 2025.
0 Comments