📌BAHATI MSANJILA.
SERIKALI imeanzisha mifumo ya ki-elektroniki katika vituo
vya Mikoa na Wilaya ili kurahisisha upatikanaji wa hati za safari, ikiwa ni
sehemu ya juhudi za kuondoa usumbufu kwa raia wa Tanzania wanapohitaji vibali
kwa ajili ya kushiriki shughuli za kijamii nchini za jirani.
hayo yameelezwa Bungeni Jijini
Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo
alipokuwa akijibu swali la Mhe. Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo
aliyeuliza Je, lini Serikali itaondoa usumbufu wa kupata vibali na gharama
pale raia wa Tanzania wanapolazimika kushiriki shughuli za kijamii nchini
Zambia.
Akijibu, swali hilo Sillo ameeleza kuwa, Serikali imetekeleza mifumo ya ki-elektroniki katika ngazi za Mikoa na Wilaya
ili kurahisisha upatikanaji wa hati za safari, pasipoti, na hati za dharura
Lengo ni kuwaondolea wananchi usumbufu wanapohitaji vibali vya kushiriki
shughuli za kijamii katika nchi jirani .
Vilevile, Mhe. Sillo amesema kuwa
raia wa Tanzania wanaoishi katika maeneo ya kilometa 10 kutoka mpaka wa
Tanzania wanapewa vibali maalum kwa ajili ya kushiriki shughuli za
kijamii, kama misiba na matukio ya dharura, bila gharama kubwa.
Ameongeza kwa kusema kuwa Kwa
raia wanaoenda nchi jirani kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, wanapaswa kufuata
Sheria na Taratibu za nchi hiyo, pamoja na kulipia vibali vinavyohusiana na
shughuli zao.
Hatua hii ya mifumo ya
ki-elektroniki ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha huduma kwa wananchi na
kuondoa changamoto za urasimu, huku pia ikifungua fursa za kiuchumi kwa raia wa
Tanzania wanaoshiriki shughuli mbalimbali katika nchi jirani.
0 Comments