VIJANA ZAIDI YA 1,000 WA UVCCM WAFANYA MATEMBEZI KUUNGA MKONO UTEUZI WA RAIS SAMIA NA DKT. MWINYI.

 ðŸ“ŒBAHATI MSANJILA

VIJANA zaidi ya 1,000 wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wamefanya matembezi maalum kuunga mkono maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika Januari 18 na 19, 2025, jijini Dodoma.

Katika mkutano huo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Mwinyi walipitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza baada ya matembezi hayo, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Kawaida, amesema vijana wamejipanga kuhakikisha viongozi hao wanapata kura nyingi katika uchaguzi mkuu akisisitiza kuwa matembezi hayo ni ishara ya msimamo wa vijana katika kuhakikisha ushindi wa CCM.

Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Jokate Mwegelo, ameongeza kuwa matembezi hayo ni sehemu ya ahadi ya vijana kuunga mkono maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu.

Amesema vijana wako tayari kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola na kuleta ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.

Vijana walioshiriki matembezi hayo wameeleza kuridhishwa na uteuzi wa viongozi hao na kuwataka wanachama wa CCM kuunga mkono maamuzi hayo.

Wamesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. Samia na Dkt. Mwinyi, kazi kubwa imefanyika, na hivyo wanastahili kupewa nafasi ya kuendelea kuongoza ili Tanzania iendelee kustawi.

Aidha, vijana hao wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kuzitangaza kazi nzuri zilizofanyika chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia, ili kuhakikisha CCM inaendelea kuaminika na kushika dola.




 

Post a Comment

0 Comments