RAIS wa serikali ya
mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ally Mwinyi ameipongeza benki ya NMB kwa kuweka
michezo kuwa ni moja ya sera ndani ya benki hiyo kwa lengo la kutoa ajira
kupitia sekta hiyo pamoja na kusaidia kuimarisha afya za watanzania.
Rais Mwinyi ameyasema hayo kwenye Mazoezi ya viungo yaliyofanyika Kisiwani Pemba, ikiwa ni sehemu ya shamla shamla kuelekea sikukuu ya mapinduzi zanzibar ambapo benki ya NMB ndio mdhamini mkuu wa maadhimisho hayo ya miaka 61 ya mapinduzi visiwani humo
Akiongea mara baada ya kumaliza mazoezi yakiwemo matembezi yaliyoanzia eneo la Kinyasini na kuishia kwenye viwanja vya Mnazi mmoja, mjini Wete, mkoa wa Kaskazini Pemba , Rais Dkt Mwinyi amesema watanzania wengi hivi sasa wanasumbuli na magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo kisukari na magonjwa ya moyo, hivyo kitendo cha NMB kuweka sera ya kusaidia michezo nchini ni mchango mkubwa katika kuokoa afya za watanzania ambazo zipo hatarini kutokana na kusumbuliwa na magonjwa yasiyoambukiza
Kwa upande wake meneja wa NMB Kanda ya Zanzibar Naima Said Shaame amesema benki ya NMB haiangalii faida tu, inaangalia pia maendeleo ya watanzania kwa ujumla wake, maendeleo ambayo hayawezi kupatikana kama afya za wananchi hao ni dhaifu , ndio maana moja ya vipaumbele ndani ya benki hiyo ni kusaidia michezo kwenye ngazi zote .Benki ya NMB imeedelea kuahidi kuwa 2025 itaendelea kushiriki kwa karibu kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi zinazoratibiwa na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na zile za Serikali ya mapinduzi Zanzibar kiwamo sekta ya michezo.
0 Comments