SERIKALI ya mapinduzi
Zanzibar imesema unapoongelea mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea kutokea
visiwani humo huwezi kuiacha kando benki ya NMB, kutokana na mchango na
jitihada zake za kuunga mkono sera za kiuchumi zinazotekelezwa na serikali hiyo
ikiwamo, miradi mikubwa ya kimkakati.
Makamu wa Pili wa Rais serikali ya mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kufungua tawi jipya la benki ya NMB WETE, Wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba, na hivyo kufanya benki hiyo sasa kuwa na matawi makubwa manne na madogo matano , pamoja na ATM 22 visiwani Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na benki ya NMB kwenye Technolojia kumewezesha ongezeko kubwa la huduma za kifedha jumuishi viwani humo na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa benki ya NMB kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Mkuu wa fedha wa benki hiyo Juma Kimori, amesema lengo la benki ya NMB ni kuhakikisha kila mtanzania popote pale alipo anafikiwa na huduma za kibenki (financial inclusion), hivyo ufunguzi wa tawi hilo la WETE ambalo litakuwa na uwezo wa kutoa huduma zote za kibenki.
Amesea ufunguzi wa tawi hilo unakwenda kufanya benki hiyo sasa visiwani Zanzibar kuwa na jumla ya matawi makubwa manne na madogo matano, ATM 22, pamoja na mawakala 721, nguvu kubwa ikielekezwa kwa watanzania kutumia mifumo ya kiteknolojia ya huduma za kifedha iliyowekwa na benki hiyo ikiwamo NMB mkononi.
Pamoja na ufunguzi wa tawi jipya la WETE pia benki ya NMB imekabidhi vifaa vya sekta ya elimu na afya kwa makamu wa pili wa rais kwaajili ya kisiwa cha Pemba, ikiwa ni sehemu ya kurudisha sehemu ya faida kwa jamii, vyote vikiwa na thamani ya sh million 110.
Takwimu zilizotolewa na Benki kuu ya Tanzania kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa Tawi jipya la Wete, Kaskazini Pemba zinaonyesha kuwa hadi sasa Zanzibar ina jumla ya benki kubwa kumi na nne, nne kati ya hizo zikiwemo kisiwani Pemba, jumla ya matawi 44, tisa kati ya hayo yakiwa Pemba, hali inayoonyesha ukuwaji wa kasi wa sekta ya kifedha na uchumi visiwani humo.
0 Comments