📌BAHATI MASANJILA
KATIBU wa Itikadi na
Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makala, leo amezungumza na waandishi
wa habari jijini Dodoma, akitoa taarifa kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa
chama hicho unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025.
Makala amefafanua kuhusu
mchakato wa uchaguzi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, akisisitiza
kuwa nafasi hiyo haiombewi wala hawajazwi fomu. Badala yake, jina la mgombea
linapendekezwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na kisha kuwasilishwa kwa
Mkutano Mkuu kwa ajili ya maamuzi ya mwisho.
Niwaombe wanachama wa CCM kuachana na taharuki zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mrithi wa Makamu Mwenyekiti, nafasi hii inapendekezwa na siyo kugombewa,” alisema Makala, akiongeza kuwa mchakato huo unazingatia misingi ya demokrasia ya chama na utaendelea kwa kuzingatia utaratibu na Katiba ya chama.
Akizungumza kuhusu
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa CCM, Makala amesema kuwa vikao vya Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa vitakutana tarehe 16 Januari 2025 kwa ajili ya
kujadili na kufanikisha maandalizi ya ajenda za mkutano.
Mkutano Mkuu wa CCM
utajadili masuala mbalimbali, ikiwemo kupokea ripoti za utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya chama kati ya mwaka 2022 na 2025, na kujadili kazi zilizotekelezwa
na chama katika kipindi
0 Comments