📌BAHATI MSANJILA
NAIBU Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano
waTanzania Doto Biteko ambae pia ni Waziri wa Nishati amezindua mikopo kwa
wasambazaji nishati safi nchini inayotolewa na benki ya NMB, huku akibainisha
wazi kuwa kukosekana kwa mitaji kwa wasambazaji wa nishati hiyo ni moja ya
kikwazo cha kampeni hiyo iliyoasisisiwa na rais wa jamuhuri ya muungano wa
Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Benki ya NMB imetenga jumla ya shillingi billion mia moja
kwaajili ya mikopo kwa wasambazaji wa nishati safi na salama, mikopo
inayotolewa kwa riba ya asilimia moja kwa mwezi huku kiwango cha juu cha mkopo
huo kwa mfanyabiashara mmoja kikiwa shillingi billion moja, lengo likiwa
nishati hiyo iweze kufika kila kona ya tanzania..
Naibu waziri mkuu ambae pia ni waziri wa nishati, amesema
tafiti zilizofanyika toka kuanza kwa kampeni ya matumizi ya nishati safi na
salama hapa nchini wamebaini kuwa moja ya sababu inayokwamisha ufanisi wa
kampeni hiyo ni kutokuwepo kwa vituo vya kuuzia nishati safi ambavyo vipo
karibu na wananchi hasa maeneo ya vijijini, hivyo kitendo cha benki ya NMB
kuanza kutoa mikopo hiyo kwa wasambazaji wa nishati safi, inakwenda kutatua
tatizo hilo .
Kwa upande wao benki ya NMB kupitia afisa mtendaji mkuu wake
Ruth Zaipuna amesema benki imetenga shilling billion mia moja za mikopo
ili upatikanaji wa nishati safi kwa watanzania uwe wa rahisi na kwamba
mkopo huo huo ambao kiwango cha juu cha mkopaji ni billion moja utalipwa ndani
ya miaka miwili, riba kwa mwezi ikiwa ni asilimia moja.
Katika kuhakikisha watanzania wengi Zaidi wanafikiwa na
nishati safi na salama, benki ya NMB kwa kushirikiana na Tais Gas wataendesha
kampeni ya kuelimisha watanzania kupitia NMB KIJIJI DAY, ambapo kwa mwaka 2025
wanatarajia kuvifikia jumla ya vijiji 2000.
0 Comments