📌BAHATI MSANJILA
WATUMISHI wa umma nchini wameeleza changamoto zinazowakabili, zikiwemo mazingira duni ya kazi na ukosefu wa usawa katika utekelezaji wa haki zao, wakati wa Mkutano Mkuu wa TUGHE uliofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali
na Afya (TUGHE) , Ndg. Hery Mkunda, amesema changamoto hizo zimeathiri utendaji
kazi wa watumishi na kuzitaka mamlaka husika kuzitatua. “Kanuni ya F.22(c),
ambayo inazuia baadhi ya watumishi kushiriki kwenye vyama vya wafanyakazi,
inakiuka haki za msingi za kazi,” alisema Mkunda.
Changamoto nyingine ni pamoja na uhamisho usio
wa lazima wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi, ukiukwaji wa sheria za mabaraza
ya wafanyakazi, na ukosefu wa rasilimali kwa Idara ya Kazi.
Mkutano huo, ulioshirikisha viongozi wa
serikali, umetoa mapendekezo kadhaa, ikiwemo kufanyia marekebisho sera
zinazozuia haki za watumishi na kuimarisha mazingira ya kazi ili kuongeza tija.
Akihutubia mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu Zuhura
Yunus amegusia masuala mbalimbali yaliyoibuliwa na Katibu Mkuu wa TUGHE, Ndg.
Hery Mkunda, ikiwemo uwepo wa vifungu vya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma
vinavyowazuia baadhi ya watumishi kujiunga na vyama vya wafanyakazi.
Hili ni suala linalojadilika Pendekezeni mapendekezo yenu rasmi serikalini ili tuangalie namna ya kufanya marekebisho, kuhakikisha watumishi wengi zaidi wanapata nafasi ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi na kufaidi huduma zenu.Aidha ameahidi kufuatilia changamoto ya baadhi ya waajiri kuwahamisha viongozi wa matawi ya vyama vya wafanyakazi kwa nia ya kudhoofisha ushawishi wao.
Amesema serikali itatoa mwongozo mpya utakaokuwa na lengo sawa na Waraka wa Watumishi wa Serikali wa mwaka 1976, lakini ulioboreshwa kuendana na mahitaji ya sasa.
Katika hotuba yake Naibu Katibu mkuu amekiri
changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa sekta binafsi, ikiwa ni pamoja na
ajira zisizo na staha, mikataba ya muda mfupi, na ukosefu wa huduma za hifadhi
ya jamii na bima ya afya.
Serikali italizingatia suala hili kwa kuongeza bajeti na idadi ya wakaguzi wa kazi ili kuhakikisha ukaguzi wa mazingira ya kazi unaboreshwa
0 Comments