WAZIRI wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, ameuagiza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa weledi na kuzingatia maelekezo yanayolenga kufanikisha mpango wa bima ya afya kwa wote nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
mifumo ya kidigitali na mpango wa Toto Afya kadi, Waziri amesisitiza umuhimu wa
kuimarisha huduma za Bima ya afya kwa wananchi.
Kama taasisi, mnatakiwa kuhakikisha mnapanua wigo wa wanachama, kuongeza ubora wa huduma, na kuondoa changamoto zinazolalamikiwa na wananchi bila kuathiri uhai wa Mfuko. Pia hakikisheni mnatoa taarifa kwa wakati ili kuepusha usambazaji wa taarifa zisizo sahihi
Waziri.
Aidha, Waziri Mhagama amekemea
vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma na wanachama.
Tabia ya kutumia Mfuko kujipatia mapato yasiyo halali haivumiliki. NHIF ituletee ripoti ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wa vitendo hivi ili kulinda uhai wa Mfuko
Katika tukio hilo, NHIF imezindua
mifumo ya kidigitali inayolenga kuboresha huduma kwa wanachama na watoa huduma.
Mifumo hiyo inajumuisha Mfumo wa Usajili wa Wanachama, unaomwezesha
mwananchi kujiunga na kujihudumia kupitia mtandao, Mfumo wa
Uwasilishaji na Uchakataji wa Madai, ambao umeunganishwa na zaidi ya
asilimia 80 ya vituo vya afya nchini.
Waziri Mhagama pia amezindua
mpango wa TOTO Afya ulioboreshwa, ambao unaruhusu watoto kujiunga na bima kwa
makundi au mmoja mmoja iwapo hawapo shuleni Mpango unaolenga kupunguza
gharama za matibabu kwa familia nyingi na kuwahamasisha wananchi kusajili
watoto wao.
Mifumo hii itarahisisha upatikanaji wa huduma, kupunguza gharama kwa wananchi na kuongeza ufanisi wa utendaji wa Mfuko.
Mfumo wa usajili utawaruhusu
wanachama kujihudumia wenyewe kupitia simu au mtandao bila kufika ofisini, huku
mfumo wa uchakataji madai ukipunguza muda wa ulipaji wa madai kutoka siku 90
hadi wastani wa siku 45,” alisema Dkt. Isaka.
Akitoa tathmini ya utendaji wa
NHIF, Dkt. Isaka amesema kuwa kati ya Julai 2023 na Oktoba 2024, Mfuko ulifanikiwa
kusajili wanachama wapya 839,331 na kufikia jumla ya wanachama wachangiaji
1,359,772. Hii imesababisha ongezeko la wanufaika wa bima ya afya hadi milioni
5.1, sawa na asilimia 8.4 ya Watanzania wote.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Afya na UKIMWI, Mhe. Elibariki Kingu amesema ustahimilivu wa sekta ya
afya na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni msingi wa kuimarisha amani na
utulivu nchini.
Amesisitiza kuwa Bima ya afya ni
muhimu kwa maisha ya kila Mtanzania, kwani inatoa uhakika wa upatikanaji wa
huduma bora za matibabu kwa gharama nafuu, jambo ambalo linaweza kupunguza
msongo wa maisha kwa wananchi.
Mhe. Kingu ameishauri NHIF
kuimarisha kitengo chake cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT) ili
kuongeza uwezo wa kufuatilia na kudhibiti vitendo vya ubadhilifu kuanzia ngazi
za chini na kueleza kuwa mifumo ya kisasa na ufuatiliaji wa karibu ni nyenzo muhimu
za kuhakikisha uadilifu na ufanisi katika utendaji wa Mfuko huo.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa
NHIF kuhakikisha bei za vifurushi vya Bima ya afya vinakuwa rafiki kwa hospitali
zote, za umma na binafsi. AMEsema usawa huu wa gharama utasaidia kuboresha
ushirikiano baina ya NHIF na watoa huduma za afya, hivyo kuhakikisha wananchi
wanapata huduma bora popote walipo nchini.
Uzinduzi wa mifumo hiyo na mpango
wa Toto Afya Kadi unatarajiwa kuwa hatua muhimu katika kuhakikisha upatikanaji
wa huduma bora na za haraka kwa wanachama wa NHIF, huku ukichochea
ushirikishwaji wa wananchi wengi zaidi katika mfumo wa Bima ya afya nchini.
0 Comments