MSIGWA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KULINDA UTULIVU WA TAIFA

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewahimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao kwa busara na kwa manufaa ya taifa, akisisitiza umuhimu wa sekta ya habari kama nguzo muhimu ya maendeleo ya nchi.

Akizungumza leo Disemba 12, 2024 Jijini Dodoma wakati wa makabidhiano rasmi ya ofisi, baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Msigwa amesema sekta ya habari ni “muhimili wa nne usio rasmi lakini wenye nguvu kubwa.”

Nawaomba tushirikiane, kwa sababu tuna kazi kubwa ya kufanya. Kalamu zetu zinaweza kubadilisha upepo wa taifa wakati wowote. Ni muhimu kutumia nguvu hiyo kwa njia inayojenga nchi yetu

Msigwa.

Ameongeza kuwa waandishi wa habari wana jukumu la kuhakikisha wanachangia utulivu wa taifa kwa kutumia taaluma yao kwa weledi.

Tanzania inahitaji utulivu. Kazi yetu sisi ni kuilinda nchi hii kwa kalamu zetu. Taifa hili linataka maendeleo, si vurugu

Msigwa.

Kwa upande wake, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Balozi Thobias Makoba, ambaye sasa anasubiri kupangiwa kituo kipya cha kazi, ameelezea mchango mkubwa wa waandishi wa habari katika kudumisha mshikamano wa kitaifa, hususan wakati wa changamoto.

Kipindi cha ajali ya kuporomoka kwa jengo Kariakoo, waandishi wa habari walionyesha uzalendo wa hali ya juu. Walihakikisha taarifa zao zinatoa uelewa sahihi na kuzuia hofu au machafuko

Makoba.

Makoba pia amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kumuamini tena na kumteua kuwa Balozi, akiahidi kuendelea kufanya kazi



Post a Comment

0 Comments