SERIKALI kupitia Wizara
ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema inatarajia kujenga chuo
Mahiri cha TEHAMA (Digital Technology Institute) Nala Dodoma, lengo
likiwa ni kusaidia kuchochea ukuaji wa
sekta hiyo nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa, leo Disemba 5,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Silaa amesema ujenzi wa chuo hicho ni wanatekeleza agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,ambapo alielekeza chuo hicho kijengwe ili kusaidia kuchochea Sekta ya TEHAMA huku akisema, kuna vijana wengi ambao wana ubunifu na kuna vyuo vikuu vingi ambavyo vinafanya bunifu, hivyo ujio wa chuo hicho itakuwa ni kituo cha kuboresha na kuwasaidia wabunifu hao.
Kazi ya chuo hicho kama nilivyosema itakuwa ni Center ya kuwasaidia vijana wengi, kampuni za vijana ambao wanakuwa na bunifu ambazo zinatoa suluhu za kitehama kwaajili ya kutatua matatizo mbalimbali ya kijamii kwenye sekta zote kama vile , kilimo sekta za afya chuo hicho kinaenda kuziba hilo pengo baina ya bunifu za vijana wetu ambao wanajitengenezea ajira zao wenyewe
Vilevile pia chuo hicho kitaweza kuwasaidia wabunifu kupata ufahamu wa sekta mbalimbali jinsi ya kufungua kampuni zao na jinsi kuweza kuwa na bunifu na bunifu zipate maeneo ya kufanyia majaribio, na chuo hiki moja ya kazi yake itakuwa ni kukusanya bidhaa za kitehama ambazo zinaweza kuuzika nje ya nchi
Silaa
Amesema mradi wa chuo hicho cha Tehama una pande mbili, chini ya mradi mkubwa wa Digital Tanzania Project ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia na umesaidia katika masuala ya uaandaji wa mtaala na majadiliano mbalimbali wa chuo hicho.
Hata hivyo amesema mpaka sasa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepata eneo Nala Dodoma la ekari 400 na maandalizi ya mradi yanaendelea ambapo tayari upembuzi yanikifu umefanyika, na mradi upo katika hatua za mwisho za majadilino ili ujenzi uanze na ndani ya miaka miwili wanatarajia kuwa chuo hicho kitakuwa kimeshakamilika.
0 Comments