UTPC YAONGOZA MAANDAMANO YA AMANI UZINDUZI SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI KWA WANAWAKE NA WASICHANA MKOANI MANYARA

 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

KATIKA kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Leo November 25 kumefanyika maandamano ya amani ya kupinga ukatili katika Mkoa wa Manyara.

Maandamano hayo yamafanyika Asubuhi ya leo ambayo yameanzia katika viwanja vya stendi ya zamani iliyoko katika mji wa Babati Hadi katika ukumbi wa White Rose ambapo waandamanaji wametembea kwa zaidi ya km 10.

Maandamano hayo yamewashirikisha makundi mabalimbali wakiwemo Waandishi wa Habari, wafanyabiashara wa Mkoa wa Manyara, Wanavyuo, maaafisa usafirishaji na wadau mbalimbali.

Aidha, maandamano hayo yameandaliwa na umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwa lengo la kusambaza ujumbe katika jamii wa kupinga vitendo vya ukatili kwa Wanawake na wasichana



Post a Comment

0 Comments