📌 RHODA SIMBA
SERIKALI imesema inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambapo katika mwaka 2023/24 ilikamilisha miradi saba kati ya miradi tisa iliyokuwa imepangwa kutekelezwa kwa kipindi hicho.
Hayo yamesemwa leo Novemba 01, 2024 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri maji Mhandisi Kundo Mathew, wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbinga mjini Jonas Mbunda ambapo amesema katika mwaka fedha 2024/25 jumla ya miradi minne imepangwa na inaendelea kutekelezwa na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Mkakati mahususi wa Serikali ni kuhakikisha inapeleka fedha zinazohitajika kwa wakati sambamba na kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maji kote nchini ikiwemo Wilaya ya Mbinga, ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi
0 Comments