📌 RHODA SIMBA
NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema kupitia bajeti Kuu
Serikali ya mwaka 2023/24 Serikali ilitoa msamaha wa kodi ya ushuru wa forodha
(customs duty) asilimia 25 kwa injini za magari yanayotumia gesi asilia
yanapoingizwa nchini.
Kapinga ameyasema hayo leo Novemba 06, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Tendega aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali kupunguza baadhi ya kodi kwenye magari yanayotumia mfumo wa gesi ili Watanzania wengi waweze kuyaagiza.
Tuaendelea na hatua mbalimbali za kuhamasisha sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye viwanda vinavyo tengeneza vipuri vinavyotumika katika kufunga mfumo wa matumizi ya gesi asilia kwenye magari na mitambo hapa nchini
Kuhusiana na usambazaji wa umeme Vijijini, Vitongojini na kwenye mitaa Mhe. Kapinga amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati imejidhatiti kuhakikisha maeneo yote nchini yanapata huduma ya umeme.
Aidha, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,Ester Matiko aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali katika kubadili magari yanayotumia mfumo wa dizeli kwenda kwenye gesi, Kapinga amesema Serikali inaendelea kuwekeza kwenye vituo zaidi ili kuhakikisha pia na magari yanayotumia dizeli yanaanza kutumia mfumo wa gesi.
Ameongeza kuwa., Mitaa ya Tampori na Chemichemi itapatiwa umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme kwenye Vitongoji 15 kwa kila Jimbo.
Kapinga amesisitiza Serikali kupitia TANESCO na REA inaendelea kuratibu kazi za kusambaza umeme katika mitaa ya Kwamtwara, Chandimo, Dumi, Hachwi na Guruma kulingana na upatikanaji wa fedha.
0 Comments