PSSSF YAWANOA WASTAAFU WATARAJIWA.

 






📌NA MWANDISHI WETU

IMEELEZWA kuwa kustaafu kumekuwa mwanzo wa changamoto mpya za kifedha na kiusalama, ambapo wastaafu wengi wamekuwa wahanga wa matapeli na mikakati ya ulaghai.

Licha ya kuwa kustaafu ni hatua muhimu na yenye matarajio makubwa yakunufaika na kufurahia matunda ya kazi kwa miaka mingi.

Akifungua semina ya maandalizi ya kustaafu leo Novemba 11, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, amewaasa wastaafu watarajiwa kuwa makini kwenye uwekezaji kwa kuepuka utapeli kwani fedha wanazopata ni nyingi kama zikiwa na malengo zinaweza kutumika kwenye uwekezaji na kutoa fursa za ajira.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu PSSSF Mbaruku Magawa, amesema kuwa Mpango huo wa mafunzo kwa Wastaafu watarajiwa wa Mfuko hufanyika kila mwaka, kwa lengo la kuwaanda wanachama wanaokaribia kustaafu waweze kutumia pesa zao vyema katika uwekezaji wenye tija ili kumudu maisha mapya ya ustaafu. 

Tangu kuanzishwa kwake Agosti 2018, Semina hii kwa wastaafu watarajiwa ni ya tatu hivyo kufanya jumla ya wastaafu 3,340 wanatarajiwa kuwa wamefikiwa baada ya kukamilika kwa semina hii 

Amesema mfuko umekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanachama wake wote katika mwaka wa Fedha 2023/24 jumla ya waajiri 746 kati ya waajiri 981 walifikiwa na tayari katika mwaka huu wa fedha 2024/25 jumla ya waajiri 207 kati ya waajiri 878 wanatarajia kufikiwa,"amesema. 

 Aidha amesema kuwa Mfuko una jukumu la kuandikisha wanachama, kukusanya michango, kuwekeza michango maeneo yenye tija na kulipa mafao kwa wanachama. 

Mfuko unalipa mafao mbalimbali yaliyoainishwa katika sheria kama vile Mafao ya uzeeni, Mafao ya Ulemavu, Mafao ya kifo, Mafao ya Wategemezi, Mafao ya kukosa ajira, Mafao ya ugonjwa na Mafao ya Uzazi 

Mafao ya uzeeni yanayolipwa kwa wastaafu yakitumika vizuri yanaweza kutoa mchango katika kuendeleza miradi mbalimbali, kutengeneza ajira kwa vijana, kuongeza pato la mstaafu na hatimaye pato la Taifa,Mfuko tangu kuanzishwa kwake tayari umelipa jumla ya mafao yenye kiasi cha shilingi trilioni 10.46 kwa wanufaika 310,458,"amesema.

Elizabeth Shayo,Msemaji Mkuu wa jeshi la polisi David Misime,pamoja na Sebastian Wambusa wamewashauri PSSSF iwe inatoa elimu hiyo mapema na si kusubiri mtu anapokaribia kustaafu.








Post a Comment

0 Comments