NMB YAZINDUA MASTABATA LA KIBABE MILIONI 300 ZATENGWA KUWAZAWADIA WATEJA

 


📌 BAHATI MSANJILA

Benki ya NMB imezundua msimu wa sita wa MASTABATA, ujulikanao kwa jina la  MASATABATA LA KIBABE, ambapo benki imetenga Jumla ya million mia tatu kwaajili ya zawadi mbalimbali, zikiwemo fedha taslimu kwa wateja na wateja watarajiwa wa benki ya NMB ambao watatumia card zao za NMB MASTERCARD kufanya miamala mbalimbali. 

Akiongea kabla ya kuzindua rasmi msimu wa sita wa MASTABATA, Afisa mkuu wa biashara na wateja binafsi benki ya NMB Filbert Mponzi, amesema lengo kuu la benki ya NMB kuendesha kampeni hiyo kwa mwaka wa sita mfululizo sasa, ni kuendelea kuhamasisha na kuwaelimisha watanzania kuachana na utamaduni wa kutumia fedha taslimu katika kufanya manunuzi mbalimbali na badala yake watumie card zao za benki na hivyo kuliwezesha taifa kushiriki kwenye uchumi wa dunia wa kidigitali ambao hautoi nafsi kubwa kwa matumizi ya fedha taslim. 

Kilichofurahisha zaidi ni bahati nasibu iliyochezeshwa kwenye ufunguzi huo wa kampeni ya MASTABATA msimu wa sita iliyofanyika kwenye maduka yaliyopo kwenye majengo ya Mlimani City jijini dar es salaam, mbapo wateja wa benki ya NMB waliokuwa na kadi za NMB MASTER CARD waliruhusiwa kushiriki, huku washindi watatu waliojinyakulia kuponi zilizowataka dani ya sekundi 45 wawe wamechagua bidhaa zenye thamani ya sh laki tatu, kwenye moja ya duka lililopo mlimani city na hapa wanaelezea uzoefu waliopata baada ya kushinda kuponi hizo na kuchagua zafado. 

Kampeni hiyo ya MASTABATA LAKIBABE msimu wa sita inayoendeshwa na benki ya NMB, ambalo litadumu kwa muda wa miezi mitatu, na ambalo lengo lake kuu ni kuwahamasisha watanzania kuachana na matumizi ya fedha taslimu na badala yake watumie kadi katika kufanya manunuzi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uchumi wa kidigitali, itakuwa na zawadi za kila wiki, zawadi za kila mwenzi na kwenye draw ya mwisho watapatikana washindi sita ambao wao na wenza sao watakwenda Dubai kwa siku tano huku gharama zote za safari Yao zikilipiwa na benki ya NMB.






 



Post a Comment

0 Comments