📌 RHODA SIMBA
MBUNGE wa
Kisesa Luhaga Mpina, amerejea bungeni mara baada ya kumaliza kutumikia adhabu
yake ya kutohudhuria vikao 15 aliyopewa na Kamati ya Maadili ya bunge na kupata
wasaa wa kuuliza swali la nyongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Leo Novemba 7,2024 Mpina ameibana Serikali ieleleze ina mkakati gani wa haraka wa kuhakikisha vijiji zaidi 6000 ambavyo havina zahanati na vijiji vingine vina maboma ya Zahanati hazijakamilika ujenzi vikamilike ili wananchi wapate huduma.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Festo Dugange amesema Serikali inathamini huduma za afya kusogezwa kwa wananchi na maeneo yote yenye sifa ya kujengwa zahanati yalishaainishwa ili utekelezaji uendelee.
0 Comments