WAKALA wa usajili wa
Biashara na Leseni (BRELA) imeendelea kuendesha mafunzo ya umiliki bunifu kwa vyuo na Taasisi za
elimu ya juu ikiwemo vyuo vikuu, vyuo vya kati na vyuo vya ufundi stadi
lengo likiwa ni kutoa elimu ya miliki bunifu.
Akizungumza leo Novemba
26,2024 mara baada ya kuendesha mafunzo katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
Afisa usajili kutoka BRELA Stanslaus Kigosi amesema wameamua kufanya mafunzo
hayo kwenye vyuo kwa kuwa wanaamini kwenye taasisi za elimu pamoja na vyuo vya
ufundi ndipo kunapopatikana ubunifu wa kila namna, kwakuwa ndipo walipo watafiti na wanafunzi
wanaojifunza, na katika kujifunza kwao
wanaibuka na ubunifu wa namna mbalimbali.
Wakati mwingine wao hawatambui kuwa huo ni ubunifu na ni mali na unaweza kulindwa kwaajili ya kuwaingizia kipato kwa mtu mmoja mmoja na taasisi zao ndio maana sisi leo tumeona tuendeshe mafunzo haya huku
Kigosi.
Nae Mhadhiri kutoka Taasisi
za Taaluma na Maendeleo UDOM, Benta Matuka amesema kupitia mafunzo hayo
wamejifunza mambo mbalimbali yanayohusu BRELA, na kwamba kwa kuwa zamani hakuwa anafahamu taratibu za kufuata
pindi mtu akiwa anataka kusajiri biashara yake.
Kingine nilichojifunza ni kwamba kumbe kusajili shughuli za kitafiti kusajili bidhaa ambazo zimezalishwa zina hatua mbalimbali lakini ni field mbalimbali, na mwanzoni nilikuwa sijui kuhusu copyright kitu gani kiende," elimu niliyoipata hapa itaniwezesha kuwafundisha masuala muhimu namna ya kusajili idea zao walizo zivumbua.
0 Comments