WAZIRI SILAA AZINDUA ZAHANATI YA IGONIA SINGIDA, IKIJIBU MAHITAJI YA HUDUMA ZA AFYA KWA WAKAZI WA MKALAMA

 

BAHATI MSANJILA


📌 BAHATI MSANJILA

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Jerry William Silaa  amezindua Zahanati ya kijiji cha Igonia, kilichopo katika Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida. 

Zahanati hii ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi mwaka 2013, ambapo Serikali ilichangia kukamilisha ujenzi wake kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 80.

Tangu kuanza kwa shughuli zake mwezi Juni, zahanati hiyo imehudumia wakazi 880, huku ikitoa huduma muhimu kwa jamii ya watu 1,408 kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, Waziri Silaa alisisitiza kwamba zahanati hiyo inajibu changamoto kubwa waliyokuwa wakikumbana nayo, ambapo walilazimika kutembea zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma za afya.

Zahanati hii inavifaa vya kisasa ambavyo vitasaidia kuwahudumia wananchi kwa urahisi, bila ya kuwa na haja ya kutembea umbali mrefu kwenda maeneo mengine kutafuta huduma, 

Waziri Silaa pia alitoa wito kwa wakazi wa kijiji cha Igonia kuisimamia zahanati hiyo ili iweze kuendelea kutoa huduma bora. 

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, alihakikishia wananchi kwamba serikali itasimamia zahanati hiyo ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa jamii.






Post a Comment

0 Comments