TGDC YAELEZEA MIPANGO UZALISHAJI UMEME ENDELEVU NA RAFIKI WA MAZINGIRA

 





  📌RHODA SIMBA

IMEBAINISHWA  kuwa Nishati ya Jotoaridhi ni endelevu, salama na rafiki wa mazingira na ina faida ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kutoa umeme bila kuzalisha gesi chafu,kutoharibu mazingira kama ilivyo kwa vyanzo vingine vya nishati na uwezo wake wa kutoa umeme kwa kasi na kwa kiwango kikubwa. 

Hayo yameelezwa na Meneja Mkuu wa kampuni ya uendeshaji Jotoaridhi Tanzania(TGDC) Mhandisi Mathew Mwangomba leo Oktoba 2,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika kongamano la 10 la jotoaridhi Afrika (ARGeo-C10) litakalofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 27 Oktoba.  

Amesema kuwa kwa sasa TGDC imeanisha takribani maeneo 52 katika mikoa 16 ambapo Tanzania inauwezo(potential) wa kupata megawati zaidi ya elfu tano za nishati ya umeme na nishati ya joto elfu kumi na tano kwaajili ya matumizi ya moja kwa moja.

Kampuni hii inaendelea na miradi yake mitano ya kipaumbele ambayo inalenga kuzalisha MW 200 za umeme

Miradi hiyo ni ngozi 70MW (mbeya),kiejo-mbaka 60MW (Mbeya),Natron 60 MW (Arusha),songwe 5MW (Songwe) na Luhoi 5-38MW (Pwani) na kufanya jumla ya Megawati 200 ambapo tunaishukuru Serikali kutuwezesha kununua mtambo wa kuchoronga visima vya utafiti vya Jotoaridhi

 Aidha amesema kuwa mtambo huo umegharimu shilingi bilioni 13.18 na utatumika kuchoronga katika mradi wa ngozi na mradi miradi mbalimbali ya Jotoaridhi nchini.

Mhandisi Mwangomba amesema, uchorongaji wa visima vya utafiti katika mradi wa ngozi unatarajia kuanza muda mfupi kutoka sasa baada ya kukamilika kwa taratibu za manunuzi. 

Kadhalika amesema kuwa kupitia miradi hiyo Tanzania inalenga kupunguza tegemezi lake kwa nishati ya mafuta, gesi na maji kuimarisha usambazaji wake wa umeme. 

Tanzania imedhamiria kuwa na umeme wa uhakika na usalama ambao hauathiriwi na madadiliko ya tabianchi kwani nishati hiyo haina masika wala kiangazi

Hata hivyo inaelezwa muwa Mkutano huo utasaidia upigaji wa hatua katika kuikamirisha safari ya jotoardhi ulimwenguni.






 


Post a Comment

0 Comments