📌BAHATI MSANJILA
Benki ya NMB imeingia makubaliano ya ushirikiano na chuo kikuu cha dar
es salaam, makubaliano yanayolenga ukuzaji wa vipaji na ujuzi kwenye sekta ya
TEHAMA , huku wakilenga zaidi maendeleo ya sekta ya kifedha ambayo ndio
kichocheo kikuu cha uchumi wa nchi.
Akiongea muda mfupi kabla ya utiaji saini hati ya makubaliano hayo, ya ushirikiano kati ya NMB na chuo kikuu cha Dar es salaam, hafla iliyofanyika makao makuu ya benki ya NMB, afisa mkuu rasilimali watu benki ya NMB Emmanuel Akonaay, akiongea kwa niaba ya afisa mkuu wa benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema benki ya NMB pamoja na kutoa kipaumbele katika kuisaidia serikali kwenye sekta ya elimu, wameweka mkazo zaidi katika kuinua kiwango cha sekta ya rasilimali watu ili nchi iweze kuwa na wataalamu wenye ubora, na hivyo ni moja ya sababu zilizopelekea benki kuingia ushirikiano huo wa miaka mitano na chuo kikuu cha dar es salaam.
Katika kuhakikisha elimu ya Tanzania inaboreka, na nchi inakuwa na rasilimali watu wenye ubora unaokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa, benki ya NMB imekuwa ikifadhili program mbalimbali kwenye vyuo vya elimu ya juu hapa nchini ikiwamo programme ya "NURU YANGU" kupitia NMB Foundation, ufadhili wa programme za kukuza vipaji vyuo vikuu mbalimbali nchini, utoaji wa nafasi ya elimu kwa vitendo ndani ya benki kwa wanafunzi wanatoka vyuo vikuu nchini pamoja na utaoaji wa mikopo ya elimu yenye riba ya asilimia tisa ambapo benki imetenga jumla ya shilling billion 200.
0 Comments