📌BAHATI MSANJILA
WATANZANIA wamehimizwa kujiwekea akiba kwenye taasisi za kifedha
ikiwamo benki ya NMB, kwakufanya hivyo itawawezesha kufanya shughuli zao za
maendeleo kwa haraka, na kufikia malengo waliojiwekea lakini pia kukopesheka
kirahisi na taasisi za kifedha, kutokana na historia ya kifedha aliyojiwekea
kwenye benki husika.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam, Dkt. Toba Nguvila ametoa wito huo kwa watanzania muda mfupi kabla ya kuzindua kampeni ya "BONGE LA MPANGO" inayoendeshwa na benki ya NMB, Kampeni yenye lengo la kuendelea kuwajengea utamaduni watanzania wa kupenda kujiwekea akiba, kwenye taasisi za kifedha hasa benki ya NMB, kampeni itakayodumu kwa miezi mitatu na kushirikisha wateja wa benki hiyo na wale tateja watarajiwa.
Dkt Nguvila amesema, Benki ya NMB wakati wote imekuwa na ndoto ya kuhakikisha inawaondolea umaskini watanzania, ikiwamo kuwainua wafanyabiashara, ndio maana imekuja na kampeni hiyo ambayo inamlenga kila mtanzania.
Kwa upande wao benki ya NMB Kupitia afisa mkuu wa wateja binafsi na biashara benki ya NMB Filbert Mponzi, wanasema benki ya NMB ni benki kinara kwenye sekta karibu zote za taasisi za kifedha hapa nchini, hivyo moja ya wajibu wake ni kuendelea kuwaelimisha watanzania umuhimu wa kujiwekea akiba kwenye taasisi za kifedha ili waweze kufikia malengo na ndoto za maendeleo wanayokusudia
Kampeni ya Bonge la mpango mchongo ndio huu"ambayo imezinduliwa rasmi na benki ya NMB, na ambayo itakwenda kwa muda wa miezi mitatu, inawahusisha watanzania wote, na ili ushiriki unachotakiwa kufanya ni kujiwekea akiba kwenye akaunti yako ya NMB kuanzia shilling laki moja, na kwa wale ambao bado si wateja wa benki hiyo wanachotakiwa ni kufungua akaunt na kuweka akiba.
Katika kampeni hiyo itakayoendeshwa nchi nzima na benki ya NMB zawadi mbalimbali zitakuwa zinatolewa kila wiki Za fedha taslim ambapo washindi kumi kila mmoja atajinyakulia sh laki moja na washindi wengine tisa watajinyakulia vifaa vya ndani, kutakuwa na washindi wa mwezi wanne ambao kila mmoja atajinyakulia sh million tano, na kwenye draw kubwa ya mwisho kutakuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo zana za kilimo pamoja na mshindi mkuu atakayejinyakulia sh million mia moja.
0 Comments